Monday, August 3, 2009

JUMUIYA YA WATANZANIA UAE (DUBAI)

JUMUIYA YA WATANZANIA UAE(TANZANIA ASSOCIATION IN EMIRATES (TAE)
Utangulizi:
Jumuiya ya Watanzania UAE ni jumiya ya hiari ya Watanzania wanaoishi na kufanya kazi katika Muungano wa falme za Kiarabu ( United Arab Emirates)
Harakati za kuunda Jumuiya hii zilianza miaka mitatu iliyopita, yaani mwaka 2006 kwa msaada mkubwa kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Abu Dhabi na Ubalozi mdogo uliopo Dubai. Toka wakati huo Jumuiya imekuwa ikifanya shughuli zake mabilmbali za kuweka pamoja Watanzania, na papo hapo ikiendelea kukamilisha taratibu za usajili wa kudumu serikalini.

Ni mwezi huu tu wa Juni 2009 ambapo Jumuiya imepata usajili wa kudumu kutoka serikalini, na hivyo kuiwezesha kufanya shughuli zake kikamilifu na kutekeleza malengo yake mbalimbali.

Malengo ya Jumuiya ya Watanzania UAE
  • Kuwajumuisha , kuwaunganisha na kuwakutanisha watanzania wote wanaoishi na kufanyakazi katika Muungano wa Falme za Kiarabu
  • Kuhakikisha kuwa Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu wanasaidiana katika kila hali, furaha na huzuni.
  • Kuwakumbusha Watanzania juu ya umuhimu wa Utaifa wetu nakuwakumbusha kutoa misaada ya hali na mali kwa familia zao, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote nyumbani Tanzania.
  • Kuwakumbusha wawe mabalozi wema na wazuri wa Tanzania ndani ya Muungano wa Falme za Kiaarabu kwa kuishi kwa amani na kutii sheria za nchi.
Mikakati ya Jumuiya ya Watanzania UAE ni pamoja na:
  • Kusaidia Watanzania wenye ujuzi unaohitajika ndani ya Muungano wa Falme za Kiarabu kupata fursa mbalimbali za ajira
  • Kulitangaza jina Tanzania kuwa ni nchi ya Kilimanjaro na Zanzibar ( The Land of Kilimanjaro & Zanzibar)
  • Kuwashawishi wenyeji wetu na wawekezaji kuwekeza vitega uchumi mbalimbali nchini Tanzania
  • Kuhamasisha wenyeji wetu kutembelea Tanzania kujionea vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na MLima Kilimanjaro; Mbuga maarufu za wanyama kama vile Serengeti, Ngorongoro, Selous na Visiwa vya Zanzibar.
  • Kuitangaza Tanzania kwenye Muungano wa Falme za Kiarabu kwa kualiak vikundi mbalimbali vya utamaduni, muziki na aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bongo Flavor na Taarab, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa na Vilabu mbalimbali.
Baada ya kupata usajili wa kudumu serikalini hivi sasa Jumuiya imefungua ofisi yake mjini Dubai na anuani ni:
Mtaa wa Omar lbn Al Kahatib, katikati ya Gulf Hotel na Al Sham Hotel
PO Box 126511 Dubai
Simu no. +971 4 2355666
Fax no. +971 4 2355688
E mail: tae@eim.ae
Website: www.watanzania-uae.com

Uongozi:
Jumuiya ya Watanzania UAE inaongozwa na kamati Kuu ya watu kumi na mbili 12 ambao ni:-
  1. Arch Mohammed Sharif - Mwenyekiti
  2. Mr.Mbarak Ahmed - Makamu Mwenyekiti
  3. Mr.Shabir Damji - Katibu Mkuu
  4. Eng. Issa Majid Maggidi - Naibu katibu mkuu
  5. Mr. Mohamed Manji- Mweka Hazina
  6. Mr. Hassan Ally Abri - Naibu Mweka Hazina
  7. Eng Shaban Mgido - Mjumbe
  8. Mr. Mohamed Jawad Aziz - Mjumbe
  9. Mr. Khamis Abulani - Mjumbe
  10. Eng. Abdulhamid Mhoma - Mjumbe
  11. Mr. Mohamed Abdulrasool - Mjumbe
  12. 12.Mr. Abdul Ismail - Mjumbe
Jumuiya pia inazo kurugenzi tatu za Wanawake, Mawasiliano na Jamii zinaongozwa na wakurugenzi na zikiwa na wajumbe wanne.
Wakurugenzi ni :
1. Ms. Rahma Bukhet saleh - Mkurugenzi Wanawake
2. Mr. Issaac Peter - Mkurugenzi Mawasiliano na Mahusiano
3. Mr. Abdulrahman Hussein - Mkurugenzi jamii na vijana

Jumuiya inapenda kuwakaribisha Watanzania wote kushirikiana nayo kwa njia yoyote ya manufaa ili kupeleka mbele malengo yake kwa manufaa ya Watanzania wote yaani kwa wale walio nchini UAE na huko nyumbani.
Kwahiyo jumuiya inakaribisha mawasiliano na maoni wakati wowote.

Mohammed Sharif
Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)

No comments:

Post a Comment

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL