
KANYE WEST ameshawishika mwenyewe kwa kujiona kuwa ana umaarufu kama marehemu Michael aliyetesa na kibao cha Thriller na anastahili kuchukua jina la nyota huyo mkubwa sana ambaye amekwisha fariki.
Kanye alisema, "Unajua kila mtu alikuwa anampenda na kumuheshimu Michael lakini muda umebadilika.
Inatia uchungu sana kuona kuwa Michael amekwenda, lakini kufa kwake kunatengeneza njia kwa mfalme mpya wa Pop na mimi niko tayari kuchukua ufalme huo.
Hakuna yeyote anayeweza kulinganishwa na mimi katika mauzo na anayeheshimiwa, kwahiyo jambo hilo ndilo linanifanya mimi kuchukua taji la Michael na kuwa mfalme mpya.
"Awali alikuwepo Elvis (Presley) na baadae alikuwepo Michael na sasa ni karne ya 21 ni wakati wa Kanye kutawala, Mimi ndiye mfalme mpya wa muziki wa Pop."

No comments:
Post a Comment