Tuesday, February 23, 2010
KUTOKA KWA AY na KINGS AND QUEENS
Video mpya ya KINGS and QUEENS featuring JOKATE and AMANI inabamba ile kinoma kwenye vituo vyote tangu ilipotoka. Video hii ambayo imetengenezwa na OGOPA DJs na Audio yake kurekodiwa na B. HITZ MUZIC GROUP chini ya mtaalam Hermy B. Kama alivyosema awali mkali huyu wa Bongo Fleva kuwa mwaka huu ni wa vitu vikali na vya viwango vya hali ya juu kutoka kwa AY. Pia mkali huyu amesema kuwa yuko katika maandalizi ya kwenda kushoot wimbo wa wake mwingine unaofanya vizuri redioni unaotambulika kwa jina la BED AND BREAKFAST. Video yake itashootiwa JOHANNESBURG SA na kampuni kubwa ya kule inayoitwa Film Online.
Subscribe to:
Posts (Atom)