Sunday, August 30, 2009

Uzinduzi wa album ya pili ya Alikiba ndani ya Marekani

Ali K amechaguliwa kuwepo katika tuzo za African Music Awards Europe 2009 zitafanyika UK tarehe 17 Oct, 09:
Uzinduzi wa album ya pili ya Alikiba ndani ya Marekani Album inaitwa Ali K 4Real ina tracks 17 na Intro na Autro so ni Tracks 19 amewashirikisha hawa-Abby Skillz,Ude Ude,Queen Darleen,Abdu Kiba,Mr Mim,Chidi Benz,Dully Sykes,Marlaw,Mwasiti,Geez Mabovu
Kazi Nyingi zimepigwa G RECORDZ Chini ya Producer KGT
MAJINA YA NYIMBO
1.Msiniseme
2.Mali Yangu
3.Shamba
4.Si Mzima
5.Ndio Yule
6.Miss Pain Apple
7.Karim
8.Far Away
9.Wanitesa
10.Tell Me Why
11.Najua Ni Kipi
12.Shababi
13.Hufai
14.Hadithi
15.Prince Waweru
16.Si Mzima Remix
17.Karim Remix
Uzinduzi Zanzibar Tar 16 Aug 09
Uzinduzi Dar Huenda ukawa Tar 21 Aug 09
Album inatoka sokoni J3 Tarehe 10 Aug 09

Friday, August 28, 2009

MALI MPYA IMEWASILI ZIZZOU FASHIONS

Uzi mkali ndani ya ZIZZOU FASHIONS, unaweza kuchapa jina lako nyuma ya Jezi au utauziwa zile zenye majina ya wachezaji nyota wa Ulaya ambao unawazimia kinoma.... zinapatikana pale maeneo ya Afrika sana na pia pale victoria kituo cha mafuta cha Oilcom

Haya haya wale ma Bro wa uhakika hapa ndio mambo yetu ya paper chaser yanapokamilika

Hey.... bling bling za nguvu
Mambo ya skafu pia kama kawa kwa ZIZZOU FASHIONS
Unataka kunesanesa.........

Wednesday, August 26, 2009

Ndani ya ofizi za Produza Enrique Fiqueredo

Produza Enrique Fiqueredo wa Sound Crafters ni produza mkongwe sana ambae mpaka sasa wapo juu, Amekuwa nominated mara nyingi tu katika tuzo za Kill Music Awards, kwa sasa ana nyimbo kama Dar mpaka Moro ya TMK Wanaume wimbo ambao umetamba ndani na nje ya Afrika Mashariki.
Kwa sasa kuna ngoma nimeskia Studio toka kwa TMK Wanaume na Tip Top Connection.
Stay tune kutoka kwa Enrique.
Aboubakar (Kwafujo) akiwa na Enrique Fiqueredo

Tuesday, August 25, 2009

HAPPIIIIII BITHDEI SHALUWA

WAUNGWANA LEO NI SIKU MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YA RAFIKI YETU JOSEPH SHALUWA, LEO NAKUMBUKA ANATIMIZA MIAKA KADHAA YA KUZALIWA KWAKE! TUNAMTAKIA MAISHA MAREFU, AFYA NJEMA NA BARAKA TELE KUTOKA KWA MUUMBA WETU ILI AENDELEE KUZITUMIA SIKU ZAKE NYINGI ALIZOPEWA HAPA DUNIANI KWA MANUFAA YA UMMA.......TUNAKUOMBEA SANA KATIKA SIKU HII MUHIMU.

SECRET LOVE SASA MITAANI
HIKI NDICHO KITABU CHANGU KIPYA, KINAPATIKANA MITAANI NCHI NZIMA KWA WAUZA MAGAZETI WOTE. LOVE SMS ZA KUTOSHA, LOVE STORY KALI KAMA KAWAIDA PAMOJA NA UCHAMBUZI WA MADA ZA UHUSIANO. UTAKIPENDA....KINAUZWA KWA BEI YA SHILINGI 2000 TU!

Monday, August 24, 2009

Wawaaaa Da' Flora Nducha

Jumamosi kuamkia Jumapili tulimsend off Flora Nducha aliyekuwa Mtangazaji wa Radio One na sasa yupo BBC London, Flora ni mmoja wa watu walionipokea vizuri sana wakati naingia Radio One na kunifundisha mambo mengi sana, nilifanya nae vipindi kama Chombeza, Kumepambazuka na Nani zaidi, kwa kweli nimegain mengi toka kwake.
Flora anaolewa na Mkenya na haruzi yao ni huko huko kwa Mzee Kibaki, wakati naoa Flora alishiriki kiasi kikubwa sana katika kufanikisha harusi yangu.

Friday, August 21, 2009

Habari za wanamuziki wa Majuu

Mashtaka yaliyokuwa yanawakabili JAY-Z na BEYONCE baada ya bodyguard wao kuwashambulia wapigapicha hivi karibuni walipokuwa kwenye mapumziko huko Dubrovnik, Croatia yamefutwa.
Sakata hilo lilitokea baada ya bodyguard kuwazuia wapigapicha kupata picha za wanandoa hao maarufu ambao ni wasanii wa muziki.
Katika kipande cha mkanda wa video wa tukio hilo umeonyesha mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina moja tu la Julius akipigana mweleka na wapigapicha wakati JAY-Z na BEYONCE wakiondoka kwenye Mgahawa huku Jay-Z akisema "Twende zetu, Twende zetu, achana nao." pia Jay-Z katika mkanda huo alisikika akisema "acha acha acha."
Wapiga picha watatu wanadai Julius aliwapa vitisho na kuwashambulia na kuharibu vifaa vyao kwenye tukio hilo wakati video haionyeshi kama kuna uharibifu.
Kwahiyo mlinzi huyo hatokabiliwa na mkono wa sheria na wala hatolipa faini yeyote.

--------------------------------------------------------------

Mwimbaji wa muziki wa R&B OMARION amekanusha kuhusika na kuvuja kwa habari ya kujitoa kwenye lebo ya Young Money ya rapa LIL WAYNE.
Mwimbaji huyo wakundi lililovunjika la B2K alisaini kujiunga kwenye ratiba ya lebo hiyo mapema mwaka huu kwenye msimu wa jua.
Ingawa alionekana kwenye tukio la utoaji wa zawadi la Young Money linalojulikana kama America Most Wanted Music Festival ( Tamasha la muziki unaotafutwa sana) ambalo lilimalizika wiki iliyopita.
Jana kijana huyo OMARION ambaye alitesa na kibao cha Ice Box inasemekana ameachia kibao ambacho hakijatolewa alichofanya na Lil Wayne kinachokwenda kwa jina la I Get It In ambacho kimezagaa kwenye mtandao wa Internet.
Na siku iliyofuata rapa wa lebo hiyo MACk Maine amethibitisha kuondolewa kwa Omarion kwenye crew ya Young Money.

----------------------------------------------------------------

Danadana bado zinaendelea kuhusu kuupumzisha mwili wa mfalme wa muziki wa Pop MICHAEL JACKSON kwenye nyumba ya milele.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baba wa Mwanamuziki huyo.
Hivi karibuni familia hiyo ilitangaza kuwa mfalme wa muziki wa Pop atazikwa tarehe 29 ambapo itakuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo angezikwa sambamba na wacheza sinema na wamamuziki nyota waliozikwa kwenye makaburi ya Forest Lawn Memorial Park huko Glendale, California.
Lakini tarehe hiyo imeahirishwa tana.
Baba wa Michael Mzee Joe Jackson amethibitisha kuwa yatakuwepo mazishi ya kipekee yatakayohudhuriwa na familia pamoja na marafiki wa karibu hivyo wamesogeza hadi tarehe 31/August /09 ili kutoa muda zaidi kwa familia hiyo kuandaa mazishi.
Michael alifariki tarehe 25/6/09 kwa mshtuko wa moyo.

Thursday, August 20, 2009

Mzee wa Farasi Ally Choki na Extra Bongo

Mmeniona je mwasemaje ....hapa ndio kwanza tunatambulisha ujio mpya wa Extra Bongo
Choki na Vijana wake wakilishambulia jukwaa

Wednesday, August 19, 2009

Queen wa mjini Amina Dushy

Mdau wa blog hii Queen Amina Dushy katika pozi kali
Unanicheki
Umecheki Tabasam hilo la mtoto Dushy

Celine Dion apata mimba

Mwanamuziki nyota wa muziki wa R&B Celine Dion amepata ujauzito wa mtoto wa pili.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 41 akiwa na mumewe mwenye umri wa miaka 67 wamefanikiwa ujauzito huo kwa msaada wa timu ya wataalam wa kurutubisha mimba huko jijini New York.
Gazeti moja la nchini Canada linaloandika kwa lugha ya Kifaransa lilitoa habari hizo jana lakini Celine Dion bado hajadhibitisha habari hizo za furaha.
Wawili hao ambao walioana mwaka 1994 tayari wana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 anayeitwa Rene-Charles.
Celine alishawahi kusema kwamba ataanza majaribio ya kupata mtoto mwingine wakati ziara yake ya dunia inayojulikana kama `Taking Chances' itakapomalizika mapema mwaka huu.
Nyota huyo akiongea na kipindi cha luninga kinachojulikana kama US talk show kinachoendeshwa na Oprah Winfrey alisema " Tutakwenda kujaribu kupata ujauzito baada ya ziara yangu. Tunatumaini tutapata mimba nyingine."
"Nina matumaini madogo sana. Lakini tayari tumekwisha jaaliwa kupata mtoto mmoja. Tulijaribu kwa miaka 6 kwa ajili ya kumpata mtoto Rene-Charles, Tuna mtoto wa miujiza."
Mume wa Celin ana watoto watatu aliowazaa katika ndoa zake zilizopita kabla ya kumuona Celine.

Monday, August 17, 2009

PAMBA KALI NDANI YA ZIZZOU FASHIONS STORE

Kama unataka kupendeza na jezi za wachezaji wa Ulaya basi hapa ndi kwao
Mikwaju mikali ya kutokea washua....

KwafujoJunior akiwa ndani ya ZIZZOU Fashions....Jamaa kibao walikuwa wanamuulizia kapotelea wapi huyu jamaa sasa huyo hapo.

Patashika ya ligi ya Uingereza

Mchezaji wa timu ya Chelsea Didier Drogba (Kulia) akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya timu ya Hull City.
Mchezaji wa timu ya Manchester United Wayne Rooney (Kushoto) akimfunga kipa wa Birmingham City Joe Hart wakati wa mechi ya ligi ya Uingereza iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Mchezaji wa timu ya Arsenal William Gallas akiruka juu na kufunga bao la kichwa dhidi ya timu ya Everton.

Monday, August 10, 2009

Ujio mpya wa Xtra Bongo

Ally Choki Mzee wa Farasi akionyesha Dole tupu kuashiria mambo kuwa sasa yameiva. Hapo alikuwa na vijana wake wa kazi ambao wanajianda kuliteka jiji kwa staili ya aina yake (kwa pembeni yake ni Kwafujo mwenyewe).

Ni wiki endi hii- Kwafujo nilipotembelea kambi ya Extra Bongo pale Mwananyamala, Bendi ipo tight usisikie pia nimesikiliza wimbo mmoja unaitwa "Mjini Mipango", vijana wametulia sana.
Alhamisi ya wiki hii watafanya Listening Party wadau kibao wa mjini wamealikwa na Ma Pedsheee kibao kama vile Chief Kiumbe, Ustadh Juma, Masoud Wanani watakuwepo kuskiza ujio mpya wa Xtra Bongo next level, Kwafujo nitakuwepo kuwaletea yaliyojiri.
Wewe endelea kublogisha tu....
Tunajifua kinoma.......
Upo hapo....hiii haijawahi tokea tutatisha ile mbaya
.........Twende sasa Extra Bongo next level tunatisha ile mbaya .....See U soon over there

Sunday, August 9, 2009

Ndani ya MJ Records

Marcochali akiwa na Kwafujo baada ya kumtembelea studio pale Mj Records Masaki.
Eee... bwana nilisikiliza mikono mikali kutoka kwa wasanii kama FID Q, Mwana FA, QJ na Makamua, halafu kuna Dem mmoja anaitwa Najma nae anakuja na ngoma moja kali sana....endelea kublogisha.
Mcheki Marcochali alipokuwa mdogo kwanye picha ya T- shirt
T-Shirt ya nani pamoja na nembo yake ni kali kuliko ya mwenzie..........

Saturday, August 8, 2009

Mwanzo wa Week end Hii

AY ......Aboubakar(Kwafujo) unatisha mshkaji wangu, mambo yako si mchezo
Kutoka kushoto ni: Oscar Makoye mchora katuni za Tall, Dogo, Usitake ncheke nk, My self Kwafujo(Abou), Mzee Ndamalya na mwisho ni DJ D-White.
Abou akiwa na akina Keisha (Female vocalist), Chege, Madee, babu Tale na Producer Macochali wa MJ Record.
Halloooo mko wapi........???????????
Aboubakar akiwa na Salama Jabir
Me, My self and ......Irene wa EATV

Friday, August 7, 2009

Rihanna kufanya show ya kwanza

Mwanadada mrembo na nyota wa muziki wa mahadhi ya R&B Rihanna atafanya onyesho kwa mara ya kwanza kwenye umati wa watu tangu aliposhambuliwa na Chris Brown miezi sita iliyopita.
Mwimbaji huyo aliyejizolea umaarufu na kibao chake cha 'Umbrella' ataonekana kwenye show ya 'The Jay Leno mwezi wa tisa tarehe 14 akiwa sambamba na nyota wa muziki wa Hip Hop Kanye West na Jay-Z.
Muunganiko huo wa mastaa hao watatu unatarajiwa kuimba single mpya inayokwenda kwa jina la 'Run This Town'.
Tom Cruise pia yuko kwenye majadiliano ya kuwepo kwenye onyesho hilo.
Rihanna, mwenye umri wa miaka 21, alishuka umaarufu wake tangu aliposhambuliwa na aliyekuwa mchumba wake Chris Brown mwezi wa pili mwaka huu.
Chris alipatikana na hatia kwa kumshambulia mwadada huyo mwezi wa sita na kuhukumiwa kifungocha miaka 5 katika uangalizi na siku 180 za kufanya kazi za kijamii pamoja na kufagia pembeni ya barabara na pia ametakiwa kuhudhuria masomo yanayohusu kukataza unyanyasaji wa majumbani.
Pia amekatazwa kumkaribia Rihanna kwa umbali wa yard zipatazo 50.
Lakini mwana dada huyo hivi karibuni alitangaza kwamba anataka amri ya mahakama ishushwe kwa Chris hadi kufikia daraja la kwanza ambapo itakuwa na mkazo zaidi.
Mwanasheria wa Rihanna Donald Etra alisema: Amri hiyo itamzuia Chris kumsumbua, kumyanyasa au kumshambulia Rihanna.
Amri hiyo itakuwa na ulinzi kamili kwa Rihanna.
Hukumu ya Chris ilipangwa kusilikizwa siku yaJumatano ya tarehe 5/08/09, lakini aliahirishwa hadi tarehe 27/8/09 baada ya Jaji kusema kuwa halidhishwi na vigezo vya amri ya kufanya kazi za kuisaidia jamii.


Michael Jackson kuzikwa Hollywood
Familia ya Michael Jackson imesemekana kuwa imewasilisha nyaraka za kufanya mazishi ya mfalme wa muzuki wa Pop katika makaburi ya Hollywood
Maofisa wa kampuni inayohusika na mazishi ya Forest Lawn Memorial Park ya Los Angeles sasa wako tayari kuanza maandalizi ya mazishi.
Ni majuma sita yamepita sasa tangu mfalme huyo wamuziki wa Pop alipofariki kwa mshtuko wa moyo.
Uamuzi huo unaonekana utamchukiza kaka wa Michael ambaye ni Jermaine ambaye alikuwa anataka Michael akazikwe kwenye viwanja vya jumba lake la zamani la Neverland, huko Santa Barbara, California.
Katherine ambaye ni mama wa Michael amekataa na kusisitiza kuwa mtoto wake kamwe hakutaka kurejea tena kwenye jumba hilo la Neverland ambalo alilitelekeza baada ya hukumu yake ya kunyanyasa watoto kijinsia ya mwaka 2005 kumalizika.
Eneo la Forest Lawn ni mahali pa mapumziko ya mwisho kwa watu maarufu kadhaa akiwemo Bette Davis, Lucille Ball, Liberace na David Carradine.
Bibi wa Michael pia alizikwa hapo mwaka 1990.

Thursday, August 6, 2009

Unamkumbuka Teacher?

Unamkumbuka Mr Teacher kakayake Profesa J unakumbuka ngoma kama Stop killing na ya hivi majuzi inaitwa muheshimiwa Rais?
Mengi kutoka kwake very soon endelea kublogisha na Kwafujo

Ladha kumi za Bongo- Radio One, na Abby Dee!

Kila Jumamosi saa 12:00 Jioni hadi saa 1:00 usiku

Jumamosi iliyopita Msimamo ulikuwa hivi
10:Uko Nae - Ismail
09:Mama Mia - Q-Chillah
08:Wanaume Kazini- TMK wanaume Famili
07: Homa ya Penzi - Sharks ft Vumi
06:Pesa - Madee ft Tunda
05:Usiende kwa Mganga - Cassim
04:Unapenda Nini - Jaffarai
03:Usife Moyo - Johson & Jackson
02:Kwa Ajili Yako - Hussein Machozi
01: Leo - AY ft Wahu

Ili kupiga kura rekodi yeyote iliyo kwenye chati izidi kufanya vizuri, itoke na ipi iingie katika chat mama, tuma maoni yako E-Mail: ladhakumizabongo@radio1.co.tz

Au tuma maoni yako hapo chini(Comment):

Tuesday, August 4, 2009

Dallys akiwa na Aboubakar Sadiq (Kwafujo)

Kwa jina kamili Naitwa Joseph Dismas Dallma(Dallys)
Aina ya Muziki naofanya ni R&B pamoja na Hip Hop kapuka.
Nilizaliwa Mwanza (Rock City) na elimu yangu nikapatia Mwanza.
Kuhusu Muziki ni kwamba niliupenda toka utotoni mpaka sasa nikaona nitimize malengo yangu kwani muda mwingi nilikuwa Nairobi na Kampala kimuziki.
Nilifanya rekodi kama Move oyamama na pii pii
Uganda na pia Kenya katika studio za 4play records.
Kwa mwaka huu nimefanya nyimbo na Jumanne Iddy Produzer akiwa ni Double B.
Na nyingine inaitwa Ushauri ambayo nimemshirikisha Taqwa toka studio za G Records KGT.
Mwaka huu natarajia kufanya vizuri mashabiki wangu wanisubiri kwa shauku.
Video zangu nafanyia katika Kampuni ya SPK Videoz iliyopo Jijini Dar.
Matarajio yangu ni kujikita zaidi katika soko la ndani na nje ya nchi kanda ya nyimbo inayotamba kwa jina la Ushauri, watu watarajie ushauri mwingine toka kwa Dallys muda si mrefu ni hayo tu.
Aboubakar Sadiq (Kwafujo) katika mapozi ya picha akiwa na Dallys
DJ BIKE katika mapozi ya picha akiwa na Dallys
Niwakati wa Lanchi Hozee Ndamalya hataki mchezo kwenye maswala ya misosi hapo ni tatu bila

Monday, August 3, 2009

"KANYE WEST Mfalme mpya wa Pop"

KANYE WEST amejitangaza kuwa yeye ndiye Mfalme mpya wa muziki wa Pop kwa kusema kuwa yeye ndiye mtu sahihi anayestahili kutwaa taji la MICHAEL JACKSON na ameamua kujitangaza mwenyewe kama "Mfalme Mpya wa Pop".
KANYE WEST ameshawishika mwenyewe kwa kujiona kuwa ana umaarufu kama marehemu Michael aliyetesa na kibao cha Thriller na anastahili kuchukua jina la nyota huyo mkubwa sana ambaye amekwisha fariki.
Kanye alisema, "Unajua kila mtu alikuwa anampenda na kumuheshimu Michael lakini muda umebadilika.
Inatia uchungu sana kuona kuwa Michael amekwenda, lakini kufa kwake kunatengeneza njia kwa mfalme mpya wa Pop na mimi niko tayari kuchukua ufalme huo.
Hakuna yeyote anayeweza kulinganishwa na mimi katika mauzo na anayeheshimiwa, kwahiyo jambo hilo ndilo linanifanya mimi kuchukua taji la Michael na kuwa mfalme mpya.
"Awali alikuwepo Elvis (Presley) na baadae alikuwepo Michael na sasa ni karne ya 21 ni wakati wa Kanye kutawala, Mimi ndiye mfalme mpya wa muziki wa Pop."

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL