Wednesday, August 19, 2009

Celine Dion apata mimba

Mwanamuziki nyota wa muziki wa R&B Celine Dion amepata ujauzito wa mtoto wa pili.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 41 akiwa na mumewe mwenye umri wa miaka 67 wamefanikiwa ujauzito huo kwa msaada wa timu ya wataalam wa kurutubisha mimba huko jijini New York.
Gazeti moja la nchini Canada linaloandika kwa lugha ya Kifaransa lilitoa habari hizo jana lakini Celine Dion bado hajadhibitisha habari hizo za furaha.
Wawili hao ambao walioana mwaka 1994 tayari wana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 anayeitwa Rene-Charles.
Celine alishawahi kusema kwamba ataanza majaribio ya kupata mtoto mwingine wakati ziara yake ya dunia inayojulikana kama `Taking Chances' itakapomalizika mapema mwaka huu.
Nyota huyo akiongea na kipindi cha luninga kinachojulikana kama US talk show kinachoendeshwa na Oprah Winfrey alisema " Tutakwenda kujaribu kupata ujauzito baada ya ziara yangu. Tunatumaini tutapata mimba nyingine."
"Nina matumaini madogo sana. Lakini tayari tumekwisha jaaliwa kupata mtoto mmoja. Tulijaribu kwa miaka 6 kwa ajili ya kumpata mtoto Rene-Charles, Tuna mtoto wa miujiza."
Mume wa Celin ana watoto watatu aliowazaa katika ndoa zake zilizopita kabla ya kumuona Celine.

No comments:

Post a Comment

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL