Friday, August 21, 2009

Habari za wanamuziki wa Majuu

Mashtaka yaliyokuwa yanawakabili JAY-Z na BEYONCE baada ya bodyguard wao kuwashambulia wapigapicha hivi karibuni walipokuwa kwenye mapumziko huko Dubrovnik, Croatia yamefutwa.
Sakata hilo lilitokea baada ya bodyguard kuwazuia wapigapicha kupata picha za wanandoa hao maarufu ambao ni wasanii wa muziki.
Katika kipande cha mkanda wa video wa tukio hilo umeonyesha mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina moja tu la Julius akipigana mweleka na wapigapicha wakati JAY-Z na BEYONCE wakiondoka kwenye Mgahawa huku Jay-Z akisema "Twende zetu, Twende zetu, achana nao." pia Jay-Z katika mkanda huo alisikika akisema "acha acha acha."
Wapiga picha watatu wanadai Julius aliwapa vitisho na kuwashambulia na kuharibu vifaa vyao kwenye tukio hilo wakati video haionyeshi kama kuna uharibifu.
Kwahiyo mlinzi huyo hatokabiliwa na mkono wa sheria na wala hatolipa faini yeyote.

--------------------------------------------------------------

Mwimbaji wa muziki wa R&B OMARION amekanusha kuhusika na kuvuja kwa habari ya kujitoa kwenye lebo ya Young Money ya rapa LIL WAYNE.
Mwimbaji huyo wakundi lililovunjika la B2K alisaini kujiunga kwenye ratiba ya lebo hiyo mapema mwaka huu kwenye msimu wa jua.
Ingawa alionekana kwenye tukio la utoaji wa zawadi la Young Money linalojulikana kama America Most Wanted Music Festival ( Tamasha la muziki unaotafutwa sana) ambalo lilimalizika wiki iliyopita.
Jana kijana huyo OMARION ambaye alitesa na kibao cha Ice Box inasemekana ameachia kibao ambacho hakijatolewa alichofanya na Lil Wayne kinachokwenda kwa jina la I Get It In ambacho kimezagaa kwenye mtandao wa Internet.
Na siku iliyofuata rapa wa lebo hiyo MACk Maine amethibitisha kuondolewa kwa Omarion kwenye crew ya Young Money.

----------------------------------------------------------------

Danadana bado zinaendelea kuhusu kuupumzisha mwili wa mfalme wa muziki wa Pop MICHAEL JACKSON kwenye nyumba ya milele.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baba wa Mwanamuziki huyo.
Hivi karibuni familia hiyo ilitangaza kuwa mfalme wa muziki wa Pop atazikwa tarehe 29 ambapo itakuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo angezikwa sambamba na wacheza sinema na wamamuziki nyota waliozikwa kwenye makaburi ya Forest Lawn Memorial Park huko Glendale, California.
Lakini tarehe hiyo imeahirishwa tana.
Baba wa Michael Mzee Joe Jackson amethibitisha kuwa yatakuwepo mazishi ya kipekee yatakayohudhuriwa na familia pamoja na marafiki wa karibu hivyo wamesogeza hadi tarehe 31/August /09 ili kutoa muda zaidi kwa familia hiyo kuandaa mazishi.
Michael alifariki tarehe 25/6/09 kwa mshtuko wa moyo.

No comments:

Post a Comment

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL