Saturday, September 19, 2009

MISS EAST AFRICA 2009- VITU ADIMU BABAKE

Sefora Messele Ghebreezgabiheir
Date of Birth 19-09-1991
Height 180
Hobbes swimming, reading

Selamawit Zerabruck Ghebreslassie
Date of Birth 19-08-1991
Height 172
Hobbes reading, Traveling, movies

------------------------------------------------------------------------------------------
Mwaka jana Nchi ya Eritrea pia ilikuwa ya kwanza kutangaza wawakilishi wake katika mashindano ya Miss East Africa 2008 yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ambapo iliwakilishwa na warembo Rahwa Ghebrehiwet pamoja ya Menal Hussien ambapo Rahwa Ghebrehiwet alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu.

Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa huandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.

Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, visiwa vya Seychelles, Re union, Madagascar, Comoros na Mauritius.

Wakati huohuo ile bahati nasibu ya Miss East Africa ya kuchangia yatima ambapo mshindi wa kwanza atajishindia gari jipya aina ya Range Rover sport inaendelea
na watu wote wameombwa kushiriki bahati nasibu hiyo.

“Tunawaomba watu wote washiriki kwa kuandika neno SHINDA kwa kutumia simu zao za mkononi na kutuma kwa sms kwenda namba 15567 ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali na wakati huohuo wakichangia yatima wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”


No comments:

Post a Comment

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL