Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE Arch. Mohammed Shariff wakiwa na baadhi ya akinamama waliohudhuria karamu ya kufuturu
Baadhi ya wadau waliohudhuria karamu ya kufuturu akiwemo mchezaji maarufu No.5 ambaye ni mstaafu wa vijana wa Msimbazi Simba, Bw. Ishaka Kibene katikati waliosimama.
Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh wa pili kulia akiwa pamoja na baadhi ya Masheikh waliohudhuria karamu. Sheikh Muhidin Abdulraham wa kwanza kushoto, Sharif Hussein Badawi wa pili kushoto na Sheikh Twalib wa kwanza kulia ambaye ni Imam wa Msikiti Maamur uliopo Upanga Dar es Salaam.
Maggidi wakiwa kwenye bango la shirika la ndege la watani wa jadi KQ
Jumuiya ya Watanzania UAE ilifanya karamu ya kufuturu pamoja Watanzania wanaoishi, kufanyakazi na waliokuwa matembezini UAE.
Watanzania toka Emirates za Abu Dhabi, Ajman, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah na Umm Al Quwain walijumuika kwenye karamu hiyo iliyofanyika Ofisi za Ubalozi Mdogo uliopo Dubai.
Pamoja na mahunjumati ya kumwaga pia kulikuwepo na tombola ya tiketi ya ndege ya Dubai - Dar - Dubai iliyotolewa kwa hisani kubwa ya shirika la ndege la watani wa jadi Kenya Airways ambao walishiriki kwenye udhamini wa karamu hiyo. Mshindi wa tiketi hiyo alikuwa Bibi Naima R. Nassor.
No comments:
Post a Comment