Friday, August 7, 2009

Rihanna kufanya show ya kwanza

Mwanadada mrembo na nyota wa muziki wa mahadhi ya R&B Rihanna atafanya onyesho kwa mara ya kwanza kwenye umati wa watu tangu aliposhambuliwa na Chris Brown miezi sita iliyopita.
Mwimbaji huyo aliyejizolea umaarufu na kibao chake cha 'Umbrella' ataonekana kwenye show ya 'The Jay Leno mwezi wa tisa tarehe 14 akiwa sambamba na nyota wa muziki wa Hip Hop Kanye West na Jay-Z.
Muunganiko huo wa mastaa hao watatu unatarajiwa kuimba single mpya inayokwenda kwa jina la 'Run This Town'.
Tom Cruise pia yuko kwenye majadiliano ya kuwepo kwenye onyesho hilo.
Rihanna, mwenye umri wa miaka 21, alishuka umaarufu wake tangu aliposhambuliwa na aliyekuwa mchumba wake Chris Brown mwezi wa pili mwaka huu.
Chris alipatikana na hatia kwa kumshambulia mwadada huyo mwezi wa sita na kuhukumiwa kifungocha miaka 5 katika uangalizi na siku 180 za kufanya kazi za kijamii pamoja na kufagia pembeni ya barabara na pia ametakiwa kuhudhuria masomo yanayohusu kukataza unyanyasaji wa majumbani.
Pia amekatazwa kumkaribia Rihanna kwa umbali wa yard zipatazo 50.
Lakini mwana dada huyo hivi karibuni alitangaza kwamba anataka amri ya mahakama ishushwe kwa Chris hadi kufikia daraja la kwanza ambapo itakuwa na mkazo zaidi.
Mwanasheria wa Rihanna Donald Etra alisema: Amri hiyo itamzuia Chris kumsumbua, kumyanyasa au kumshambulia Rihanna.
Amri hiyo itakuwa na ulinzi kamili kwa Rihanna.
Hukumu ya Chris ilipangwa kusilikizwa siku yaJumatano ya tarehe 5/08/09, lakini aliahirishwa hadi tarehe 27/8/09 baada ya Jaji kusema kuwa halidhishwi na vigezo vya amri ya kufanya kazi za kuisaidia jamii.


Michael Jackson kuzikwa Hollywood
Familia ya Michael Jackson imesemekana kuwa imewasilisha nyaraka za kufanya mazishi ya mfalme wa muzuki wa Pop katika makaburi ya Hollywood
Maofisa wa kampuni inayohusika na mazishi ya Forest Lawn Memorial Park ya Los Angeles sasa wako tayari kuanza maandalizi ya mazishi.
Ni majuma sita yamepita sasa tangu mfalme huyo wamuziki wa Pop alipofariki kwa mshtuko wa moyo.
Uamuzi huo unaonekana utamchukiza kaka wa Michael ambaye ni Jermaine ambaye alikuwa anataka Michael akazikwe kwenye viwanja vya jumba lake la zamani la Neverland, huko Santa Barbara, California.
Katherine ambaye ni mama wa Michael amekataa na kusisitiza kuwa mtoto wake kamwe hakutaka kurejea tena kwenye jumba hilo la Neverland ambalo alilitelekeza baada ya hukumu yake ya kunyanyasa watoto kijinsia ya mwaka 2005 kumalizika.
Eneo la Forest Lawn ni mahali pa mapumziko ya mwisho kwa watu maarufu kadhaa akiwemo Bette Davis, Lucille Ball, Liberace na David Carradine.
Bibi wa Michael pia alizikwa hapo mwaka 1990.

No comments:

Post a Comment

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL