Wednesday, September 23, 2009

MAMBO YA SIKUKUU YA IDD




Assam akiwa na mtoto wa Masoud Wanani wakicheza hapa ni nyumbani kwa Masoud
Twende sasaaaa mnenguaji wa bendi ya Diamond Musica, Salma Bonge akiwajibika jukwaani kwenye sikukuu ya Idd.
Mnenguaji wa bendi ya Diamond Musica, Jane Costa akiwa kazini katika onyesho la Idd.
Mashabiki wa kundi la Jahazi Modern Taarab wakiserebuka katika onyesho la kundi hilo kwenye sikukuu ya Idd .

Saturday, September 19, 2009

MISS EAST AFRICA 2009- VITU ADIMU BABAKE

Sefora Messele Ghebreezgabiheir
Date of Birth 19-09-1991
Height 180
Hobbes swimming, reading

Selamawit Zerabruck Ghebreslassie
Date of Birth 19-08-1991
Height 172
Hobbes reading, Traveling, movies

------------------------------------------------------------------------------------------
Mwaka jana Nchi ya Eritrea pia ilikuwa ya kwanza kutangaza wawakilishi wake katika mashindano ya Miss East Africa 2008 yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ambapo iliwakilishwa na warembo Rahwa Ghebrehiwet pamoja ya Menal Hussien ambapo Rahwa Ghebrehiwet alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu.

Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa huandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.

Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, visiwa vya Seychelles, Re union, Madagascar, Comoros na Mauritius.

Wakati huohuo ile bahati nasibu ya Miss East Africa ya kuchangia yatima ambapo mshindi wa kwanza atajishindia gari jipya aina ya Range Rover sport inaendelea
na watu wote wameombwa kushiriki bahati nasibu hiyo.

“Tunawaomba watu wote washiriki kwa kuandika neno SHINDA kwa kutumia simu zao za mkononi na kutuma kwa sms kwenda namba 15567 ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali na wakati huohuo wakichangia yatima wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”


Thursday, September 17, 2009

Beezy kukamua kinoma ndani ya Goethe-Institut

Jamaa anatisha sana hasa kwa kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la "Get out"!
Siku hiyo atashirikiana na 7Bisha wakati mshamilishaji wa shughuli hiyo atakuwa Carola Kinasha ...... usikose tarehe 26/9/09 shoo hii kali kuliko zote!!!!!!!!!!!!!

Felix washusha pamba kali kwa ajili ya Idd el fitr

Je unataka ulipuke na pamba kali siku ya Idd el fitri... Yooo ma bro na master Du......check inside

Wednesday, September 16, 2009

Safari ya mwisho ya Mpakanjia

Wakazi wa jiji la Dar wakiwa wamebeba jeza la Meddy Mpakanjia kuelekea makaburi ya Kisutu

Monday, September 14, 2009

MTV Video Music Awards

Beyonce akila Pozi la nguvu na tuzo zake alizotwaa ikiwemo ya Video bora ya mwaka na alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kutumbuiza na kibao chake maarufu cha Single Ladies akiwa na madansa 30 wa kike ambao alikuwa amefanana nao.
Jay Z akila pozi la nguvu na kimwana Alicia Keys baada ya kufanya shoo iliyowadatisha mashabiki
Chapombe Kanye West akimnyang`anya Mic mwanadada Taylor Swift na kuanza kumfagilia malkia wa tuzo tatu Beyonce.
Nyota wa muziki wa rap Kanye Wiz akikata kilauli kwenye sherehe za MTV Video Music Awards


Friday, September 11, 2009

Maandalizi ya sikukuu ya Idd el fitr

meee meeee......pisha njia........Nani kasema mbuzi kagoma kwenda......Hapa mwendo mudundo kakubali mwenyewe na anaongoza njia kwa kuteta na dereva wake.....hahahahahaha......Maandalizi ya sikukuu ya Idd wewe utambebaje mbuzi wako? asigome kwenda?

Wednesday, September 9, 2009

Mdau wetu Mary Mwita

Mdau wetu Mary Mwita kutoka Zanzibar ni mtangazaji wa kituo cha radio cha Chuchu FM ana tangaza vipindi kama enzi zile , flava za taratibu low fire na kipindi hiki cha mfungo ana kipindi kinaitwa Dakudaku time na pia aliwahi kuwa miss Chumbageni Tanga.

Tuesday, September 8, 2009

Vidosho wa Miss Tanzania 2009

Mapozi ya baadhi ya Totoz za Miss Tanzania mwaka huu 2009

KARAMU YA IFTAAR YA WATANZANIA UAE

Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE Arch. Mohammed Shariff wakiwa na baadhi ya akinamama waliohudhuria karamu ya kufuturu
Baadhi ya wadau waliohudhuria karamu ya kufuturu akiwemo mchezaji maarufu No.5 ambaye ni mstaafu wa vijana wa Msimbazi Simba, Bw. Ishaka Kibene katikati waliosimama.
Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh wa pili kulia akiwa pamoja na baadhi ya Masheikh waliohudhuria karamu. Sheikh Muhidin Abdulraham wa kwanza kushoto, Sharif Hussein Badawi wa pili kushoto na Sheikh Twalib wa kwanza kulia ambaye ni Imam wa Msikiti Maamur uliopo Upanga Dar es Salaam.

Maggidi wakiwa kwenye bango la shirika la ndege la watani wa jadi KQ
Jumuiya ya Watanzania UAE ilifanya karamu ya kufuturu pamoja Watanzania wanaoishi, kufanyakazi na waliokuwa matembezini UAE.
Watanzania toka Emirates za Abu Dhabi, Ajman, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah na Umm Al Quwain walijumuika kwenye karamu hiyo iliyofanyika Ofisi za Ubalozi Mdogo uliopo Dubai.
Pamoja na mahunjumati ya kumwaga pia kulikuwepo na tombola ya tiketi ya ndege ya Dubai - Dar - Dubai iliyotolewa kwa hisani kubwa ya shirika la ndege la watani wa jadi Kenya Airways ambao walishiriki kwenye udhamini wa karamu hiyo. Mshindi wa tiketi hiyo alikuwa Bibi Naima R. Nassor.

Monday, September 7, 2009

Siku tulipougawa mwezi wa Ramadhan

Sasa mshkaji wangu hebu punguza bei unajua mimi nimetoka mbali hadi kuja hapa Kawe beach kwa ajili ya kitoweo cha Ftari na Daku
KwafujoJunior akipima uzito wa Samaki....."mmmh nadhani huyu anatosha kula peke yangu si unajua mambo ya Daku."

Thursday, September 3, 2009

BESTA AKANA KUHUSU MIMBA

Mwenyewe alisema hivi, "Saivi kuna uzushi umeenea kwenye vyombo vya habari kua am pregnant, nimekanusha hilo jambo c la kweli.
Sina mimba, na naendelea na music kama kawaida."
"Saiva am prepared 4 my new vdeo. wimbo unaitwa Usirudi, nafanya kwa Adam."
Says Besta.

Vyombo vya habari acheni kumzushia mrembo huyu nadhani mmesoma wenyewe alichokisema.
Endelea kujiblogisha na Kwafujo ili upate habari zake za uhakika.






Mambo Sawio Commisions Agents Co. Ltd.

Habari njema kwa Wote wenye magari waliyoyachoka wapeleke wapewe mapya, ukipitia Kwafujo mkopo upo.


Tuesday, September 1, 2009

AY ndani ya MTV Afrika Music Awards

Msanii wa muziki wa Bongo Flavour Ambwene Yesaya (AY) akiwa na Sara Kaisi akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki Tuzo za MTV Afrika Music Awards ambayo yatafanyika jijini Nairobi mwezi ujao.

THIS BLOG IS POWERED BY TRIZ MOTEL

THIS BLOG IS POWERED BY  TRIZ MOTEL